Friday, March 20, 2015
20-03-2015 Ulikuwa unajua kama leo ni siku ya FURAHA Dunia
20-03-2015 ...Tangu kuazimishwa siku ya wapendanao dunia 14-02. Leo ni siku ya FURAHA Duniani.
Mwanaume kajifanya mwanamke ili afanye kazi Bar, kilichofuatia ni story..
Ugumu wa maisha unaongeza ubunifu, ubunifu
mwingine unakuweka pabaya.. huu wa huyu jamaa
sidhani kama tunaweza kuuita ni ubunifu ila jamaa
aliamua tu atumie njia hii ili apate tu njia ya kupata
mkate wa siku.
Mmiliki wa Bar ya Siaya, Kenya alimshtukia jinsia
ya mmoja ya wahudumu wake wa Bar kwamba
jinsia yake sio ya kike.. Akatoa taarifa Polisi
kuhusu mhudumu huyo, walipokuja kumpekua
jamaa alijitetea kwamba ana jinsia mbili.
Jamaa huyo anaitwa Michael Obiero alikamatwa
baada ya kufanya kazi kwa siku mbili kwenye Bar
hiyo akijitambulisha kwa jina la Brenda na pia
alikuwa akilala chumba kimoja na wahudumu
wengine wa kike.
UKIONA HIVI HAPA LAZIMA PANA USALITI!!
1. Simu yake kaifunga kwa password.
2. Kila ukiingia inbox unakuta hakuna sms hata moja
au za kwako tu unazomtumia na za kutoka kwenye
mtandao.
3. Ukiangalia kwenye phone book yake utakuta
majina ya ajabu ajabu mengine utakuta y ama x au
kuna namba namba tu.
4. Kila mara ukimpigia simu anajifanya hakusikii na
kusema yuko kwenye kelele wakati wewe husikii
kelele.
5. Hataki ushike simu yake hata mara moja.
6. kila mkutanapo hupenda kuzima simu yake.
7. mara nyingi ukimpigia hapatikani na husingizia
simu ilikuwa imekwisha chaji na wakati anatumia
simu inayotunza chaji kwa muda mrefu.
8. Kama mtu akimpigia simu, akapokea wakati upo
ataongea naye kwa hofu na kumpa majibu ya mkato
na wakati mwingine ataogopa kutoka ili akaongelee
mbali ili umwamini kuwa anaongea na mtu wa
kawaida tu. baada ya kumaliza kuongea ukimuuliza
ulikuwa unaongea na nani atajifanya hakusikia swali
na kuitikia kwa kuguna ili urudie kuuliza wakati huo
yeye anatafuta jibu la kukudanganya.
9. ukimbananisha baada ya kuhisi anakudanganya
atajifanya na hasira na kutaka kukutishia kwa
maneno fulani ya kutaka uhusiano wenu kuvunjika.
na baadaye yanafuata maneno ya kujitetea kiujanja.
10. Kila mnapokuwa pamoja huwa anapenda
kukutungia maneno ya kukutuhumu huku akifikiri
vile anavyokufanyia ndivyo unavyomfanyia,kama
ujuavyo mtenda akitendewa....
JIPANGE!!!!!!!
MBINU ZA KITAALAM ZA KUDHIBITI USALITI
Maumivu ya mapenzi yanaelezwa kuwa ni
makali zaidi pengine kuliko kitu chochote .
Wakati fulani maumivu hayo hushinda hata yale
ya makovu ya kutapeliwa kibiashara na
mengine mengi yanayokera.
Utafiti unaonesha kwamba , wanaume ambao
wana ndoa imara na wanaishi maisha ya
furaha, wana nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa
katika maisha yao .
Utafiti huo unaendelea kueleza kwamba,
wanaume hao wawapo kwenye majukumu yao
ya kazi huwa wachapakazi zaidi kuliko wale
wenye ndoa zenye migogoro kila kukicha.
Kutokana na utafiti huo , bila shaka sasa
unaweza kuona ni kwa namna gani mapenzi
yanaweza kusababisha matatizo au mafanikio
katika maisha . Ni suala la kufahamu na
kuchagua tu.
Marafiki zangu wapenzi, leo ndiyo namalizia
mada hii ambayo imedumu hapa kwa wiki nne
mfululizo. Ingawa ni ndefu ni matumaini yangu
kwamba haijakuboa na badala yake
imekuongezea kitu .
Katika matoleo yaliyopita, nilieleza kwa mapana
juu ya usaliti na sababu zake . Kubwa zaidi
nililokazia ni namna ya kukomesha usaliti huo
ndani ya ndoa .
Yapo mengi niliyoeleza huko nyuma, leo
nitamalizia na vipengele vingine muhimu zaidi
ambavyo bila shaka vitawaongezea vitu vipya
ubongoni mwenu .
Kama mtakumbuka , nilieleza zaidi mambo
ambayo kama yakizingatiwa kwa umakini
yatasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda ndoa au
uhusiano dhidi ya usaliti.
Naomba nisisitize tena , mada hii imelenga zaidi
juu ya usaliti ndani ya ndoa . Hebu twende
tukamalizie sehemu hii ya mwisho nikiamini
kwamba utajifunza kitu .
ZUNGUMZA NAYE KUHUSU HOFU YA MUNGU
Jenga mazingira ya mwenzi wako kuogopa
Ukuu wa Mungu. Jambo hili linawezekana
ikiwa utamsisitiza au kumrejesha katika
Mamlaka ya Mungu kiimani . Mweleze kuwa
kwenda kinyume na matakwa yake ni rahisi
ndoa kubaki bila uangalizi , mwishowe shetani
kuingiza mafarakano .
Mhimize kufanya Ibada , tengeni muda wa
kusali/kuswali/ kuomba dua pamoja kabla ya
kulala na kuamka. Mweleze mustakabali wa
ndoa yenu uko mikononi mwake , utakuwa
umemjenga sana .
Kumsisitiza kuhusu kuwa karibu na Mungu,
kwake litakuwa jambo jema na utakuwa
umejiongezea thamani kwake. Atajua kwamba
yupo na mtu makini ambaye akili yake inafanya
kazi sawasawa na mwenye hofu juu ya
aliyemuumba.
Amini usiamini kwa njia hii utakuwa umejiweka
mbali na usaliti maana angalau utakuwa na
mwenzi ambaye unajua anaamini katika imani
yake sawasawa na ni mwoga wa kukosea .
SUALA LA MAGONJWA
Mustakabali wa ndoa yenu , hauwezi kuwa
mzuri kama magonjwa hatari yakiingia . Ukimwi
ni tishio , tenga muda wa kuzungumza naye
‘seriously ’ kuhusu hili.
Elewa kwamba kwa kumweleza kuhusu hatari
ya maradhi ndani ya nyumba, si kama utakuwa
unamtisha, lakini utakuwa unampa ukweli
ambao unaonekana wazi .
Suala la maradhi ya kuambukiza kwa njia ya
ngoni si jambo la kufumbiwa macho , ni lazima
lijadiliwe kwa mapana na nafasi kwa wanandoa.
Kuzungumza naye juu ya hili kutamfanya
kwanza aamini kwamba hata wewe upo
salama na unajua unachokifanya hivyo , ikiwa
yatatokea ya kutokea, yeye ndiye
msababishaji . Kwa vyovyote vile hakuna
anayependa kuonekana kuwa yeye ndiye
aliyesababisha matatizo ndani ya nyumba ,
hivyo utakuwa umesaidia kumuweka kwenye
hofu ya uaminifu.
Hii itakuwa hatua nyingine yenye faida kwako .
Kumbuka lengo kuu ni kuhakikisha kwamba
husalitiwi na mwenzi wako anakuwa mali yako
peke yako . Tuendelee kujifunza .
JUU YA WATOTO
Matokeo ya familia isiyo na masikilizano ni
mwanzo wa mwisho mbaya wa watoto , usaliti
husababisha mafarakano ndani ya nyumba na
hapo sasa ndipo mtakapoanza kuingia kwenye
hatari ya kuwatumbukiza watoto kwenye
matatizo.
Hili mnapaswa kulijadili kwa kina. Zungumza
naye sana juu ya mipango mbalimbali ya
wanenu. Onesha unawapenda na wanahitaji
sana msaada wenu kama wazazi .
Kuzungumzia kwako watoto, kutampa nguvu
kwamba yupo na mwenzi sahihi anayetumia
muda wake kufikiria familia yake . Hilo litadizi
kumfanya aachane na mawazo ya usaliti kwa
sababu ana uhakika yupo na mwanamke
sahihi. Kama ndivyo, akatafute nini nje ?
TAMAA
Tamaa ni kati ya mambo yanayosababisha
usaliti unaozaa nyumba ndogo baadaye.
Msisitize juu ya tamaa na umtake awe na
uvumilivu na mambo msiyo na uwezo nayo.
Huu ni ushauri , lakini ukiutoa kwa kumaanisha,
unaweza kujenga kitu fulani kichwani mwake
na akajikuta hashawishiki kirahisi kwa tamaa
ndogondogo.
KUNA USALITI WA BILA KUKUSUDIA?
Wapo rafiki zangu ambao wanaweza
kunishangaa kwa kuuliza kama kuna usaliti wa
bila kukusudia. Ukweli ni kwamba upo . Kama
ilivyo kuua bila kukusudia, pia kuna usaliti bila
kukusudia.
Usaliti huu hufanyika kutokana na mhusika
kujenga/kujengewa mazingira ya kufanya
hivyo. Epuka kuwa karibu na mtu ambaye mna
jinsia tofauti.
Usiruhusu mazoea sana hasa ya kuchat au
kuwa naye sehemu tatanishi . Jiheshimu na
uwe mtu wa mipaka . Anayetakiwa kukuzoea
sana ni mke/ mume wako tu.
Kuna baadhi ya watu wanakuwa na ukaribu au
utani na watu wa jinsia tofauti. Mazoea
yanapozidi huweza kukuingiza kwenye
matatizo. Kamwe usipende kuwa na utani usio
na maana na mtu wa jinsia nyingine.
Unaweza kujikuta umeingia kwenye matatizo
na mwisho wake ukabaki unajilaumu tu wakati
unaweza kupingana na tatizo hilo . Amini
usiamini, inawezakana kabisa kukaa mbali na
usaliti.
Kwanza jijenge wewe mwenyewe halafu
mfundishe na mwenzako . Kufanya hivyo
kutakufanya uishi maisha ya amani na furaha
katika ndoa yako .
Mada imeisha. Wiki ijayo nitakuwa hapa kwa
mada nyingine nzuri zaidi, NAWAPENDA SANA!
WATAALAMU WANASEMA, WANAMKE MWENYE MAUMBILE MAKUBWA (MAKALIO) NDIO HUZAA WATOTO MWENYE ......
Huzaa watoto wenye AKILI ZAIDI ama nyingi sana kama tulivyoona kwa NICE VALENTINO mwenye umri wa miaka mitatu.
Ukitaka kujua zaidi piga 0767 955 825.
Mechi ya Juzi MESSI afanya mambo ya kushangaza ulimwengu.
Mchezaji huyo ambaye ni hatari sana kwenye soka.. juzi alifanya maajabu yake zaidi na zaidi.
MVUA YATABIRIWA KUNYESHA SIKU TATU MFULULIZO...Unataka kujua lini na lini?
Matokeo ya watabiri wa hali ya hewa wamesema mvua itanyesha kuanzia tarehe 20, 21 na 22 Dae Es Salaam