1. Simu yake kaifunga kwa password.
2. Kila ukiingia inbox unakuta hakuna sms hata moja
au za kwako tu unazomtumia na za kutoka kwenye
mtandao.
3. Ukiangalia kwenye phone book yake utakuta
majina ya ajabu ajabu mengine utakuta y ama x au
kuna namba namba tu.
4. Kila mara ukimpigia simu anajifanya hakusikii na
kusema yuko kwenye kelele wakati wewe husikii
kelele.
5. Hataki ushike simu yake hata mara moja.
6. kila mkutanapo hupenda kuzima simu yake.
7. mara nyingi ukimpigia hapatikani na husingizia
simu ilikuwa imekwisha chaji na wakati anatumia
simu inayotunza chaji kwa muda mrefu.
8. Kama mtu akimpigia simu, akapokea wakati upo
ataongea naye kwa hofu na kumpa majibu ya mkato
na wakati mwingine ataogopa kutoka ili akaongelee
mbali ili umwamini kuwa anaongea na mtu wa
kawaida tu. baada ya kumaliza kuongea ukimuuliza
ulikuwa unaongea na nani atajifanya hakusikia swali
na kuitikia kwa kuguna ili urudie kuuliza wakati huo
yeye anatafuta jibu la kukudanganya.
9. ukimbananisha baada ya kuhisi anakudanganya
atajifanya na hasira na kutaka kukutishia kwa
maneno fulani ya kutaka uhusiano wenu kuvunjika.
na baadaye yanafuata maneno ya kujitetea kiujanja.
10. Kila mnapokuwa pamoja huwa anapenda
kukutungia maneno ya kukutuhumu huku akifikiri
vile anavyokufanyia ndivyo unavyomfanyia,kama
ujuavyo mtenda akitendewa....
JIPANGE!!!!!!!
No comments:
Post a Comment